Hivi
karibuni zilisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha
msanii wa Bongofleva Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ akionekana kurudi kwenye
dawa za kulevya.
Leo December 31 2016 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na mama wa Chid Benz, baada ya
kuonana na mama yake Chid Benz haya ni maneno aliyoyaandika kwenye
ukurasa wake wa Instagrm...
Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo
“Chid Benz” ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya.
Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku
wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.
Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge, wauzaji na
wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya
tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote
ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola.
Mbali ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo, ni wajibu wa kila aliye
RAIA MWEMA kutoa taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya
madawa ya kulevya.
Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada
wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya
kawaida. Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa, unaweza kutatua matatizo
yako bila kutumia madawa ya kulevya.
Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo
“Chid Benz” ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za
kulevya.Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea
huku wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya serikali
dhidi ya magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya
imeongezeka hasa katika awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais
J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua
kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola. Mbali ya vyanzo vya
taarifa tulivyonavyo,ni wajibu wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa taarifa
zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha
kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida. Unaweza
kuimba,unaweza kufanikiwa,unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia
madawa ya kulevya.
Saturday, December 31, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment