Wafugaji wa kijiji cha Changalawe kata ya Masanze wilaya Kilosa mkoani
Morogoro walioyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa na jeshi la polisi
kufuatia tukio la mkulima Agustino Mtitu kuchomwa mkuki mdomoni na
kutokea shingoni hatimaye wamerejea makazini kwao huku wakilalamikia
baadhi ya mifugo yao kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.
Wakizungumza baada ya kurejea kutoka porini walikojificha kwa siku tano
wafugaji hao wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wamesema mtuhumiwa wa
kosa la kumchoma mkuki mkulima wamemkabidhi...
kwenye mamlaka husika na
hivyo wameliomba jeshi hilo kuwaacha huru wale wasiokuwa na hatia.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa
Morogoro Ulrich Matei amesema hawatasita kuwakamata wafugaji wote
wanaoendelea kusababisha uvunjifu wa amani katika wilya ya Kilosa.
Nao baadhi ya wakulima wamesema kijiji hicho kimekumbwa na hofu kubwa na
kwamba familia ya ndugu Mtitu aliyechomwa mkuki nayo ilitoweka na
kuomba hifadhi kwa wasamaria wema.
Saturday, December 31, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment