Pages

Subscribe:

Friday, September 8, 2017

CHAMA CHA WANASHERIA NCHINI KENYA CHALAANI TUKIO LILILO MPATA TUNDU LISSU


Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimelaani vikali  tukio la kupigwa risasi Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu. Rais wa LSK, Isaac Okero amesema tukio hilo limewashtua  wanasheria wote wa Kenya kwani ni tukio la kusikitisha .

“Tumepata taarifa kwamba Lissu amepigwa risasi akiwa kwenye gari lake mjini Dodoma, kwa kweli...
imetushtua sana na inahuzunisha, Kwa pamoja tunalaani tukio hilo kwa kuwa hili limewagusa wanasheria wote wa Afrika na hata dunia kwa jumla, Tunasikitika kwa uvunjifu wa sheria uliofanyika,’’ amesema kupitia Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari jana jioni.

SOMA ZAIDI – Vyombo vya dola viwasake waliohusika tukio la Mhe. Lissu – Rais Magufuli
Mhe Tundu Lissu amepigwa risasi jana mchana na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma.

0 comments:

Post a Comment