Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili ameingilia kati ugomvi wa
Dogo Janja na Young Dee na kusema kwamba wanapaswa kushindana kimuziki
na siyo kushambuliana katika maisha yao binafsi kwani jambo hilo
linaweza kuja kuwaletea madhara kwa baadae
Nikki
wa Pili amesema hayo baada ya
kupita siku kadhaa tokea Dogo Janja kutoa kauli yake ya kukataa
kufananishwa na Young Dee kwa madai ni 'mteja wa unga' jambo ambalo...
lilizua makelele mengi kwa mashabiki wa wasanii hao pamoja na meneja
wake Young Dee.
"Mimi naona kuna tatizo
hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi, kwa hiyo
ningefurahi kuona wanashindana kimuziki zaidi. Maana unapokuwa maarufu
ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika
kiurahisi, kwa hiyo ni vizuri kuchagua maneno ya kutumia", amesema Nikki wa Pili.
0 comments:
Post a Comment