Muigizaji na mfanyabiashara wa mavazi nchini, Jacqueline Wolper
amefunguka na kudai hatamani kumuona mpenzi wake akiendelea kufanya
kazi zake za kimitindo ndani ya nchi kwa maana ameshaanza jitihada za
kumtafutia kazi za kimataifa.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu Wolper
amesema watu wanadai mpenzi wake ni mbeba pochi lakini anachojua ni...
wivu ndiyo unaowasumbua kwa sababu wanafahamu kazi anayofanya lakini kwa
kuwa yeye anathamini kazi ya mpenzi wake huyo lazima atahakikisha
anamvusha boda kwa kutumia mtandao alionao.
"Kuna mtu anamuita 'BFF'
mbeba pochi, najua anafahamu ni kazi gani anafanya lakini kwa kuwa
anaumia lazima amchafue. Mpenzi wangu ni 'model' ambaye ameshafanya kazi
nyingi tu za kutembea majukwaani lakini si unajua sekta za mitindo hapa
nyumbani?, hazijazingatiwa sana kwa hiyo mimi kwa kuwa tayari nina
'connection' nje nitampigania kuona anafanya kimataifa zaidi na siyo
nyumbani" Wolper.
Akizungumzia kuhusu mpenzi wake huyo kutumika kama mpendezeshaji video 'Video King' "Suala
la kutumika kama 'video King' hapa nchini sitaki kabisa kusikia wala
kuona kwa sababu hakuna maslahi, na mpaka sasa jiandaeni kuona 'suprise'
kwani tayari kuna 'dea'l za kazi za South Afrika tumeshasaini mikataba
kwa hiyo mambo ni mazuri upande wetu".
Mbali na hayo Wolper
amesema haogopi kumsaidia mpenzi wake kwa hofu ya kuja kusalitiwa
mbeleni kwani anaamini Mungu amempatia Brown kwa kuwa ana vigezo vyote
anavyohitaji na hata ikitokea akamsaliti hatakuwa na shida kwani atakuwa
daraja la mafanikio yake.
0 comments:
Post a Comment