Rapa Dogo Janja mwenye hit ya Ngarenaro amefunguka kama asingekuwa
mwanamuziki na kupata mafanikio basi angekuwa mwizi au sheikh kutokana
na maisha aliyoishi huko awali.
Dogo Janja
amesema kuwa kama asingefanikiwa kwenye muziki basi kwenye maisha yake
angeendelea na kuiba au angebadilika na kuwa Sheikh kwa sababu baba yake
alikuwa...
akijitahidi kumbana sana ili aweze kusoma chuo (Madrasa)
"Nilikua kibaka kweli,
Mjanja mjanja sana, lakini Mzee naye alikuwa akinikamata ananibana sana
niende madrasa. Msikiti wa Ngarenaro nilikuwa napiga adhana , hicho ni
kitu ambacho kilikuwa kinanipelekea hata nisiache kwenda Madrasa a
nilikuwa vizuri kwenye dini sema utundu na maisha ndivyo vilivyonifanya
niingie kwenye muziki" amesema.
Katika hatua nyingine Janjaro amesema
kwamba anamshukuru Mungu kwa hatua aliyofikia kwani amebadilika na sasa
amekuwa kijana anayeishi kwa kufuata misingi ya nchi na dini bado
hajaiacha.
Aidha Dogo Janja amesema kwamba kuhusu
albamu watu wakae tayari kwani hivi karibuni yeye na msanii Madee
wataachia albamu waliofanya pamoja.
"Mimi ndiyo Dogo wa kwanza
kupeleka albam kwa Mamu. Nina albamu moja inaitwa mtoto wa uswazi na ya
pili tumeshafanya na Madee ipo tayari siku siyo nyingi tunaachia mzigo" - Dogo Janja.
0 comments:
Post a Comment