Akiongea Linah amesema hajutii kwa picha alizozipiga katika
kipindi cha ujauzito wake wakwanza kwa kuwa yeye ni mtu maarufu na
aliamua kufanya kitu ambacho...
roho yake ilijisikia kufanya kwa kipindi
kile na kuongeza kwamba hata siku akibeba mimba nyingine anaweza
kufanya kitu kama hicho kwa kuwa hakikumuharibia chochote katika maisha
yake.
Hata hivyo Lina aliendelea kusema
kwamba "Binadamu ni watu wa ajabu sana na hata ufanye nini huwezi
kuwaridhisha kwa kuwa kila mtu anatamani ufanye kile anachokitaka yeye
nikivaa gauni refu watasema mimi nimshamba na hata nimevaa hizo nguo
fupi bado wanasema hazina maadili hivyo mi nafanya ninachojisikia na
waacha waendelee na malumbano yao"alifunguka.
Mbali na hayo Linah amefafanua pia suala
la watu kumuona yeye kama amechelewa kujifungua ni kutokana na
kwamba watu wengi waliwahi kufahamu hali yake mapema tangu ikiwa na
miezi mitatu hivyo walikuwa kama wanamuhesabia na ilipopitiliza wiki
ndipo walipoanza kuhoji.
0 comments:
Post a Comment