Monday, September 18, 2017
UTAFITI: WACHUNGUZI WAWEKA WAZI MADHARA YA ULAJI WA NYAMA YA NGURUWE
Utafiti unaonyesha ulaji wa nyama nyekundu una madhara makubwa sana kuliko ulaji wa nyama nyeupe hata hivyo watu ambao hawali nyama kabisa wako mbali sana na hatari hizi. Lakini kwa kua nyama pia ina faida katika miili yetu basi nyama nyeupe ni salama sana kuliko nyekundu. Hebu tuangalie madhara ya nyama kama ifuatavyo.
1. Hatari ya kupata magonjwa ya moyo:
Nyama ina kitu kinaitwa lehemu kitaalamu kama cholesterol, hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa...
kupita vizuri hii husababisha viuongo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi. Japokua cholesterol ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha hii inayoongezeka kutoka kwnye nyama ni hatari sana.[nyama nyekundu ina cholestrol nyingi zaidi]
2. Kansa ya utumbo mkubwa:
Nyama nyekundu ikiliwa inakaa masaa ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara ya haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe.
3. Ugonjwa wa kisukari:
Watu wanaokula nyama na wasiokula nyama baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi mfulululizo[cohort studies}… watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana kuliko wale wasiokula.
4. Ugonjwa wa kifafa:
Minyoo inyopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Halii hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.
5.Unene uliopitiliza:
Nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo mfano kwenye nyama ya nguruwe.unene na kitambi ni hatari sana kwana husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye swala la unene.
Hitimishao:
Nyama tunazokula siku hizi sio nyama halisi tena ukiangaliwa nyama ya kuku inayoliwa sana kwenye miji mikubwa na hotel kubwa namaanisha kuku sa kisasa, zinakuzwa kwa kemikali nyingi sana ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu na hata ladha yake ni tofauti kabisa na kuku wa kienyeji. Lakini kwasababu wamiliki wa biashara za nyama ni watu wenye fedha nyingi sana duniani ukweli huu hufichwa.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment