Msanii wa miondoko ya singeli Man Fongo
amefunguka na kudai hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kumhofia katika
kazi zake kwa kuwa wote hawajaweza kufikia kile anachokifanya yeye mpaka
sasa.
Man Fongo
amebainisha hayo baada ya kuwepo
maneno ya muda mrefu kwa wasanii wanaoimba singeli kila mmoja wao kujipa
jina la...
mfalme katika uwimbaji wa muziki huo.
"Hakuna msanii yeyote
anayeimba singeli kwamba nikimuona moyo wangu unaweza ukaingia na kitete
au hofu, kwa sababu hakuna mwenye wasifu mkubwa kama mimi 'CV',
wanatakiwa walitambue hilo. Na kama wanataka niwaogope basi kwanza
wafanye vitu vikubwa zaidi yangu, ndiyo nitaweza kuwaogopa lakini kama
huna 'CV' kama zangu bado utabakia kuwa 'kinda", amesema Man Fongo.
Kwa upande mwingine, Man Fongo
amewataka wasanii wenzake wawe wabunifu katika kufanya muziki wao ili
mradi singeli iweze kuonekana siyo muziki wa kurudia rudia maneno kila
mara.
0 comments:
Post a Comment