Pages

Subscribe:

Tuesday, September 19, 2017

Q BOY: MTU PEKEE ANAYEWEZA KUNIAMBIA SIJUI KUIMBA NI PRODUCER



Msanii wa Bongo Flava, Q Boy Msafi amesema kitendo cha kuambiwa hawezi muziki kunamfanya ajitume zaidi, Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Unaanzaje’ amesema kuwa maneno ya namna hiyo yanamfanya kuongeza juhudi katika kazi, ila ni vitu ambavyo vipo kila mahali.

“Mimi nachukulia kama changamoto kwa sababu ujue unapokuwa unasaka tonge lazima ukutane na changamoto za kukukatisha tamaa, kwa hiyo unapopata...
feedback kama hizo zinakufanya uongeze hasira na juhudi ili uweze kuprove wrong watu na vile ambavyo wanakufikiria,” amesema Q Boy.

Hata hivyo ameongeza kuwa mtu pekee anayeweza kusema hawezi kuimba ni producer na kueleza kuwa maproducer wote aliokwishafanya nao kazi akiwemo Mr. T Touch wanakubali uwezo wake.

0 comments:

Post a Comment