Rapa Farid Kubanda 'Fid Q' ameibuka na kuwachana baadhi ya wakina dada
wenye tabia ya kuwategeshea wanaume zao ili wapate watoto kwa kuwaambia
hicho wanachokifanya hakina utofauti na unyanyasaji hivyo wanapaswa
wabadilike katika hilo jambo.
Fid
Q ameeleza hayo baada ya kuwepo wimbi kubwa la wanaume kukataa kulea watoto
wao kwa kisingizio cha kusema hakuwa wamejiandaa katika...
kipindi hicho
kuwa walezi wa mtoto.
"Huo ni ukatili na dhuruma,
ongea na mtu mkubaliane na siyo umtegeshee mwenzako ili upate mtoto.
Maisha siku hizi ni magumu sana, watu wanaishi kwa mipango na ratiba
kamili ya mwaka kwa lugha nyepesi naweza sema watu wanaishi kwa
'principal'.
Kwa hiyo ushauri wangu kwa wakina dada acheni ukatili na
mjitahidi kuongea na wenza wenu ili muweze kupata kile mnachostahili
katika mahusiani yenu", amesema Fid Q.
Mbali na hilo, Fid Q amedai hata kama umri wake unazidi kusogea mbele na kuwa mzee hayupo tayari kukurupuka kuingia katika ndoa.
"Siyo kitu cha kukimbilia
maana wanasemaga bora ukosee kazi kuliko kukosea mke wa kuoa, kwa sababu
ukikosea kuchagua mke wa kuoa anaweza kukuharibia maisha yako yote. Kwa
hiyo tayari nina 'idea' na mtu ambaye anafaa kuolewa na mimi chamsingi
tu nawaomba mniombee dua za kheri, ili nasi tuone kama tutaweza kutimiza
moja ya suna kubwa za binadamu", amesisitiza Fid Q.
0 comments:
Post a Comment