Pages

Subscribe:

Wednesday, September 6, 2017

KENYATTA: NI HAKI YANGU KUIKOSOA MAHAKAMA

Rais Uhuru Kenyatta ametetea hatua yake ya kuikosoa mahakama ya juu na Jaji Mkuu David Maraga kwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais akisema ni haki yake kufanya hivyo. 

Akizungumza katika kampeni za chama cha Jubilee katika kaunti ya Kajiado jana, Rais Kenyatta alisisitiza madai yake kwamba mahakama hiyo ya juu ilipuuzia...
mbali haki ya wananchi ili 'kumfurahisha' mtu mmoja aliyemtaja kuwa mpinzani wake Raila Odinga.

Amesema, licha ya kuwa anaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo anajua kwamba alishinda uchaguzi huo kwa zaidi ya kura milioni 1.4. na kwamba, ana imani atashinda tena uchaguzi wa marudio.

0 comments:

Post a Comment