Thursday, September 14, 2017
LESOTHO WAHALALISHA KILIMO CHA MMEA AINA YA BANGI
Lesotho inakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuhalalisha kilimo cha Bangi kwa ajili ya matumizi ya matibabu na zao la kibiashara nchini humo.
Waziri wa Afya nchini humo, Nyapane Kaya amesema wamefikia maamuzi hayo baada ya tafiti zilizofanywa na Kampuni ya dawa za...
mitishamba ya Verve Dynamics ya nchini Afrika Kusini.
Kampuni ya Derve Dynamics ilipata kibali cha kimataifa cha kujaribu matibabu kwa kutumia Bangi kama dawa lakini imekuwa ikipata chagamoto ya upatikanaji wa malighafi hiyo.
Hata hivyo bangi hiyo itakayolimwa nchini humo itakuwa ni zao la biashara tu na sio kwa matumizi mengine kutokana na maelezo yaliyolewa na serikali.
“Upatikanaji kwa wingi wa bangi barani Afrika umechukua sura mpya kwani kampuni yetu Verve Dynamics imepata kibali cha kutumia mmea huo kwa matibabu na utafiti wa kisayansi na kuwa kampuni ya kwanza Afrika kupewa kibali hicho cha kimataifa na kuanza mchakato wa kuzalisha mmea huo” amesema Richard Davies Mkurugenzi wa Verve Dynamics huku akiishukuru serikali ya Lesotho kwa kuhalalisha kilimo cha zao hilo, “Uamuzi wa Serikali ni wa kihistoria unamaanisha kwamba Lesotho itafanya jukumu kubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia zao hili linalopigwa vita barani Afrika, wote kwa pamoja bila shaka tutanufaika. “
Lesotho inatajwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kwa uzalishaji wa zao hilo ambalo linapigwa marufuku na nchi zote barani Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) ya mwaka 2007, watu zaidi ya milioni 38 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 64 wanatumia Bangi huku Nigeria ikitajwa kuwa vinara wa matumizi ya kilevi hicho barani Afrika na ikiwa nafasi ya tatu duniani, ambapo asilimia 14.6 ya watu wote nchini humo hutumia bangi.
UN imekadilia kuwa Afrika inapoteza dola bilioni 78.9 za kimarekani kwa mwaka hii ni kutokana kutokuhalalisha zao hilo.
Kutokana na hali ya hewa na mazingira ya milima nchini Lesotho, inaelezwa kuwa zao hilo huenda likawa tegemezi kwa uchumi wa taifa hilo.
Baadhi ya nchi barani Afrika, kama Kenya na Afrika Kusini zimekuwa zikipigania zao hilo lihalalishwe kwa matumizi ya kawaida na kibiashara.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment