“Chidi namuheshimu kama mdogo wangu kama rafiki yangu hatujawahi kutaniana. Ni kawaida sio tusi ambalo lingeweza kunifanya...
nichukie,” amesema Madee.
Kuhusu ujumbe aliandika katika mtandao wake wa twitter; ndio maana huwa sivuti sigara. Madee amekanusha ujumbe huo kumlenga Chidi Benz.
“Hilo ndio tatizo ambalo watu wengi wanashindwa kutafsiri ndio maana huwa napenda kujiita wino mweusi naandika kitu halafu kinakuweka wewe kwenye giza haujui, mpaka unitafute mimi nikueleweshe,” ameongeza.
Suala hilo lilifikia hapo baada ya Chidi Benz kudai kuwa amefanya kolabo na Tupac ambaye kwa sasa ni marehemu kitu kilicholeta mshangao.
0 comments:
Post a Comment