Pages

Subscribe:

Tuesday, September 5, 2017

MAYUNGA AFUNGUKA SABABU ILIYO PELEKEA UKIMYA WAKE

Msanii wa muziki wa bogo Mayunga ambaye alipata fursa ya kusimamiwa na kampuni kubwa ya muziki duniani ya Universal, ametubu juu ya ukimya wake na kuwaomba radhi watanzania na mashabiki wake, na kusema kwamba uongozi wake ndio ulimkwamisha. 

Akizungumza alipokuwa akitambulisha kazi yake mpya, Mayunga amesema ukimya wake ulisababishwa na uongozi wake kutotimiza...
yale ambayo waliahidiana kwenye mkataba.

"Kwa kweli tukizungumzia ukimya kwanza ningependa kuomba radhi, ni changamoto ambazo msanii yeyote zinamkuta, hakuna msanii ambaye anapenda kukaa kimya pasipo chochote kuendelea labda kama kunakuingizia pesa, unajua hii mikataba mikubwa inakuwa na changamoto sana,  ndani inakuwa na mipango mikubwa utafurahia, lakini kwangu imekuwa tofauti, mambo mengi yalienda tofauti, walikuwa hawataki kuniachilia", alisema Mayunga.

Mayunga ambaye kwa sasa amerudi na kazi yake mpya ya 'Nawekeza', amesema kwa sasa ameachana na uongozi huo, na kuwa chini ya uongozi wa kampuni ya Trace, pamoja na baadhi ya watu wa hapa hapa nyumbani.

0 comments:

Post a Comment