Pages

Subscribe:

Thursday, September 7, 2017

MBUNGE NYALANDU AOKOA WATOTO WENGINE WAWILI

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu usiku wa jana ameweza kuokoa watoto wawili Nuru pamoja na Seif ambao walipata ajali mbaya wiki iliyopita na kupelekea kuvunjika vibaya watoto hao huku watu wengine saba wakipoteza maisha katika ajali hiyo.

Mbunge Nyalandu alifanya maamuzi hayo baada ya kupata taarifa kuwa watoto hao licha ya kuvunjika vibaya miguu lakini...
walipewa tiba za kijadi kwa kufungwa majeraha yake kwa njia za kijadi.  

"Usiku wa kuamkia leo, majira ya saa 6 usiku nilienda kijijini Ilongero na kuwachukua watoto wawili (Nuru na Seif) waliokuwa wamevunjika vibaya miguu kupitia ajali ya Lori la Mnadani wiki iliyopita. Watoto hawa walifungwa majeraha yao kwa njia za kijadi, ambako baada ya kuwafikisha hospitali ya Malkia wa Ulimwengu, Puma Wilaya ya Ikungi, sasa wamepangiwa kufanyiwa upasuaji kwa dharura" alisema Lazaro Nyalandu
Aidha Mbunge huyo anasema baada ya kufanikisha kuwafikisha hospitali watoto hao madaktari walisema kuwa wanaimani watoto hao wanaweza kutembea tena "Madaktari wamesema wana imani kuwa watoto hawa ingawa wamevunjika vibaya, wanaweza kutembea tena. Katika ajali hiyo, wasafiri wenzao 7 walipoteza maisha. Tuwaombee watoto wetu Nuru na Seif" alisema Lazaro Nyalandu
Mbunge Lazaro Nyalandu hii ni mara ya pili kwake kujitoa katika kusaidia watoto ambao wamepatwa na majanga mwezi Mei mwaka huu baada ya wanafunzi wa Lucky Vicent kupata ajali mbunge huyo aliweza kufanikisha watoto walionusurika katika ajali hiyo kupata matibabu nchini Marekani

0 comments:

Post a Comment