Rais John Magufuli amesikitishwa na taarifa alizozipata tukio la
kupigwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa
nyumbani kwake Dodoma Jana na kuviagiza vyombo vya dola viwasake
waliyofanya uhalifu huo.
Rais
Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter jioni ya jana na
kutaka...
vyombo vya usalama kuwatafuta watu waliofanya tukio hilo la
kinyama.
"Nimepokea kwa masikitiko
tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu
aweze kupona haraka. Vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na
tukio hilo la kinyama na kuwafikisha katika mikono ya sheria", ameandika Rais Magufuli.
Tundu Lissu amepigwa risasi leo mchana
akiwa yupo nyumbani kwake mjini Dodoma 'Area D' kwa ajili ya kupata
chakula cha mchana baada ya kutoka katika viwanja vya Bunge
0 comments:
Post a Comment