Pages

Subscribe:

Monday, September 4, 2017

Story: NILILALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI - 14

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (14)
ILIPOISHIA…
Nilifanikiwa kupata usingizi kiasi. Ulikuwa usingizi wa mang’amung’amu. Usingizi wangu ulijawa na ile shauku ya kuujua ukweli giza litakapopotezwa na nuru. Nilitabasamu kidogo kwa sababu mzee niliyekuwa nikimtafuta, kesho ningekutana naye katika gereza nililomwona ili ayamalize matatizo yangu.

ENDELEA KUISOMA…

Asubuhi ilifika. Jogoo liliwika kama halitaki. Nilitamani kuamka ili niende mapema gerezani kuuliza habari za Mzee Samike. Lakini nilipotaka kuinuka, akili ikaniambia...
pata usingizi wa kutosha. Lala kidogo utaamka baadaye. Nikalala.

Nilishtuka saa nane mchana. Haukuwa usingizi wa kawaida. niliiogopa hali hiyo lakini sikujali. Nikajiandaa harakaharaka kisha nikaianza safari ya kwenda gerezani.

Nilifika gerezani. Kama nilivyowaza awali, haikuwa siku ya kuwatembelea wafungwa. Sikujali. Nikamsogelea askari mmoja aliyesimama imara pembezoni mwa ukuta mnene wa jela.

“Habari yako afande,” nilitoa salamu. Afande akageuka. Alikuwa mweusi ti, kama kipande cha giza, meno meupe yaliyoacha mwanya mpana mfano wa pengo na kichwani alifanana na sufuria kwa ule ukubwa wa kichwa chake. Kilichonimaliza nguvu ni kwamba, alikuwa ni yule askari wa jana ambaye alinitega nikadondoka kisha akanifukuza.

“We kijana umerudi tena?” alihoji akiwa na mshituko.
“Ndiyo mkuu, sina ubaya wowote, nina shida tu.”
“Shida gani, halafu usinisogelee.”
“Nimekuja kumuona ndugu yangu kafungwa hapa.”
“Leo siyo siku ya kuona wafungwa kijana.”
“Hakuna tatizo afande, mfungwa mwenyewe huwa namuona akiwa nje, hivyo nadhani ni rahisi kuonana naye, nisaidie afande.”
“Nimesema leo siyo siku ya kuona wafungwa kijana. Nitakupiga ngwara nyingine, ile ya jana umeisahau siyo? Kwanza mfungwa mwenyewe anaitwa nani?”
“Anaitwa Samike.”
“Aaaaah… yule mzee kamaliza kifungo chake leo. Kaachiwa, hayupo tena hapa. Haya kijana ondoka usirudi, nikikuona tena maeneo haya nakuingiza mule, unapaona?” alisema akinionyesha ukuta wa gereza. Nilitikisa kichwa kuashiria kukubali. Kisha nikaikamata njia kurejea mahali pangu pa kupumzika.

“Atakuwa amekwenda wapi baada ya kumaliza kifungo?” niliuliza nikiwa mbali. Afande akanitazama kwa dharau kisha akajibu: “Mimi si  baba yake… ondoka kijana nisikuone!” niliondoka  kichwa juujuu na mikono nimeipachika hukohuko juu.

Mambo yalizidi kuwa magumu. Ni kweli nilikuwa katika hatua ya kumpata Samike. Lakini tatizo jipya likaibuka la mzee kumaliza kifungo chake bila kuonana naye. Nilitafakari ni wapi mzee huyu angeelekea. Nikakosa jibu.

Nililala usingizi wa matumaini. Niliamini ni lazima ningempata Samike. Nikiwa usingizini, niliota mseto wa ndoto za zamani na mpya. Katika ndoto mpya iliongezeka sura ya askari. Nilikiota kichwa chake. Nikawa kama naogelea katika ndoto za masufuria. Nilipoota kuhusu kufukuzwa, nilipiga makelele. Kama kawaida yao, wazinzi wakashtuka wakidhani ni fumanizi. Walipogundua ni mimi, kama ilivyo siku zote wakanipuuza. Mchezo wa nyama ukaendelea.

Ni wapi alikokwenda Mzee Samike baada ya kutoka jela? Popo atafanikiwa kumpata?

0 comments:

Post a Comment