Tuesday, September 5, 2017
WIZKID AWAOMBA RADHI MASHABIKI KWA KILICHO TOKEA
Msanii kutoka nchini Nigeria, Wizkid amewapigia magoti mashabiki zake kwa kushindwa kuhudhuria tamasha la muziki la Made in America (MIA)2017.
Tamasha hilo lilifanyika kwa siku mbili mfululizo maeneo ya Philadelphia, kwenye uwanja wa Benjamin Franklin Parkway. Kupitia mtandao wa Twitter, msanii huyo...
ameomba radhi mashabiki kwa kosa hilo.
“Apologies to my fans in philly! Missed made in america yesterday but will make it up in a major way! ,” ameandika Wizkid. Pia msanii huyo akawajulisha mashabiki zake kuwa ifikapo tarehe 29 mwezi huu atakuwa na tamasha lingine Uingereza hivyo wasikose.
Tamasha la MIA 2017 limeudhuliwa na muandaaji wa tamasha hilo Jay Z pamoja na wasanii kama J.Cole, Migos, Solange, Pusha T, Run the Jewels, Vic Mensa, DMX, 21 Savage,Sampha na Ugly God, Rob Stone, PnB Rock, KYLE, A Boogie Wit Da Hoodie, na wengineo
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment