Sunday, September 10, 2017
ZADII: NINAVYOISHI HUWA SIENDI CLUB WALA SINA HAYO MAISHA
Rapper wa SSK, ZaiiD amesema si kweli aliwadiss Zari na Diamond katika ngoma ya Habari ya Leo. Katika ngoma ya SSK ‘Habari ya Leo’ ambayo imewakutanisha ZiiD, Wakazi, P the Mc na Cjamoker, kuna line ZaiiD anasema, “Nipo chimbo sitaki pari, Diamond flow sitaki Zari”.
“Naposema sitaki pari kweli mimi ninavyoishi siendi club, sifanyi chochote, sina hayo maisha ambayo watu wengine wanayo. Diamond flow na wala sitaki zari mara...
nyingi nimerelate Diamond alivyo na Zari alivyo lakini pia nina flow ya diamond kwa maana ZaiiD ni mtu ambaye mara nyingi watu wanamsifia sana unaflow lakini hauendi” ameiambia Bongo5.
“Kwa pamoja ya kuwa na diamond flow lakini mimi sitaki zari kwa maana hii flow yangu itakuja kunitengenezea hela, yaani sitaki kutengeneza hela kwa zari kama wasanii wengine nataka nitengeneze kwa sababu nina uwezo,” ameongeza.
ZaiiD kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ambayo inakwenda kwa jina la Wowowo.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment