Leo March 6, 2018 Wanachama wa Shirika la Africa Diaspora Forum
wamefanya maandamano nchini Afrika Kusini kushinikiza serikali ya nchi
hiyo na ya Tanzania kubaini ukweli kuhusu kuuawa kwa mwanafunzi raia wa
Tanzania mwezi February.
Baraka Leonard Naferi, mwanafunzi wa shahada ya uzamifu, alifariki baada ya kugongwa na gari nje ya bweni la chuo kikuu. Maafisa wa shirika hilo wameandamana
kwa pamoja na baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha
Johannesburg nje ya...
bweni linaloitwa Sophiatown ambapo mwanafunzi huyo
aligongwa na kufariki.
Maandamano hayo yalikuwa salama na watu walikusanyika kwenye uzio mahali gari lilipo mgonga marehemu Baraka Naferi wakiwa wamebeba mabango yanayosema tunataka haki kwa Baraka, haki itendeke kwa Baraka.
Mtuhumiwa alikamatwa na polisi wa Afrika Kusini lakini baadaye akaachiliwa huru kwa dhamana. Polisi walisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfungulia mashtaka ya mauaji.
0 comments:
Post a Comment