Uchunguzi uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba
mastaa wengi wa sinema za Kibongo wapo katika hali ngumu kiuchumi
kutokana na soko la filamu kudorora huku wizi wa kazi zao na kusitishwa
mikataba yao na makampuni makubwa ya usambazaji vikichangia.
Uchunguzi huo umebaini kwamba moja ya makampuni yaliyositisha
mikataba ya wasanii ni...
Steps Entertainment ambao wamesababisha mastaa
kibao kushindwa kutengeneza muvi kwa kuwa awali walikuwa wakipewa bajeti
na Steps kisha kuwauzia kwa bei ya mapatano.
Ilibainika kwamba baada ya Steps kuachana na utaratibu huo na kudai
kuwa wanachukua muvi zilizoandaliwa na makampuni binafsi za mastaa
wachache kama Jacob Steven ‘JB’, Athuman Amri ‘Mzee Majuto’, Vincent
Kigosi ‘Ray’ na wengine wenye makampuni binafsi.
Mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu, Musa Issa ‘Cloud 112’ alikiri
kuwepo kwa hali hiyo huku akifafanua kuwa Steps kuna wakati inakuwa
kwenye kipindi kigumu.
0 comments:
Post a Comment