
Habari kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zilieleza kuwa tukio la Aunt kutumbuliwa lilijiri hivi karibuni ambapo staa huyo alikuwa akificha...
siri hiyo isinaswe na mapaparazi wetu, jambo ambalo limemshinda.

“Kweli gari langu limeshikiliwa na TRA ila haina tatizo sana kwani wamekagua, karibia kila kitu kipo sawa isipokuwa ninadaiwa kodi tu ambayo nayo si fedha nyingi kiasi cha kunishinda. Waliniambia vibali vyake vyote viko sawa na kwamba lipo nchini kihalali kabisa hivyo ninachotakiwa kulipia ni kodi tu ambayo najipanga kulipia muda wowote.
“Nilishtuka sana baada ya kukamatwa kwani nilihisi ndiyo mwisho wa kuwa na gari langu lakini sasa nimepata moyo baada ya kuambiwa hakuna kilichochakachuliwa.
“Natafuta Sh. milioni 10 na kitu ili niweze kulikomboa,” alisema Aunt aliyedai gari hilo alinunuliwa na baba mtoto wake, Moses Iyobo ‘Moze’ huku akigoma kutaja bei yake.
0 comments:
Post a Comment