skip to main |
skip to sidebar
MR. BLUE: COUPLE NINAYO IKUBALI ZAIDI NI YA DIAMOND NA ZARI
Rapper Mr Blue amesema Diamond na Zari ndiyo couple anayoikubali zaidi. “Ukinitoa mimi na Wahyda couple ambayo naipenda, naielewa ni Zari na
Diamond.
“Yaani wanapendeza unajua eeh, na Mungu amewajaalia wamepata mtoto,
wanashirikiana kama marafiki kwenye... biashara, wanajua kucheza na akili
za raia, wanaitengeneza couple yao ya kimapenzi, wanaifanya pia inakuwa
kibiashara, yaani very nice,” aliongeza.
Kwa upande mwingine Blue amesema hana kabisa bifu na Diamond.
“Sina bifu na Diamond na juzi tumekutana naye Mwanza kwenye show ya
Ne-Yo alivyokuja, tumeongea vizuri, tumesalimiana, safi kabisa.”
0 comments:
Post a Comment