Pages

Subscribe:

Tuesday, July 5, 2016

RAMA DEE ATOA SABABU YA KUIKUBALI SINGELI

13437361_1762653040681253_1800321275_n
Rama Dee akiwa msanii wa kwanza anayeimba ‘pure rnb’ kuimba wimbo wenye vionjo vya Singeli. Staa huyo ameiambia Bongo5 kuwa baada ya kuja Tanzania kutoka Australia alikohamishia makazi yake, alivutiwa na jinsi wasanii wa muziki wa Singeli wanavyoufarahia muziki wao.

Anasema alienda maeneo ya Kigogo, Kawe na kwingine na kugundua kuwa kuna wananchi ambao hawajui muziki mwingine zaidi ya huo na...
jinsi unavyoweza kuwa muziki unaotambulisha Tanzania.

“Mimi naamini muziki wa Singeli tunaweza tukapiga hip hop juu, tukapiga rnb, tukapiga maragga yaani kila kitu kikaenda sawa kabisa, lakini tunakuwa na sound yetu hata Mkenya akisikia anajua kabisa hii Tanzania,” amesema Rama Dee.

“Naupenda, ni muziki mzuri sana.”
Amesema ni vyema kuwashukuru pia EFM ambao wameukuza muziki huo na kuwapatia ajira vijana wengi. Kwa upande mwingine Rama Dee amesema mapokezi ya Mazoea yamekuwa makubwa hasa kutoka kwa watu wa nje.

“Walishangaa sana kwamba nawezaje kufanya vile kwasababu mimi nasound tofauti kidogo halafu muziki unasound Kiafrika kwahiyo nimechanganya kiasi kwamba mpaka sound imetoka nzuri sana,” anasema.
“Kwahiyo wanapenda sana.”

Anadai pia ameshangaa kuona watanzania wanaupenda muziki huo na kwamba ni vyema wakaupa support kwasababu ndio future. Kwa upande mwingine mkali huyo wa rnb amesema Young Yuda aliyemshirikisha ni msichana na sio mvulana kama watu wengi wanavyodhani

0 comments:

Post a Comment