Pages

Subscribe:

Friday, November 18, 2016

BABY MADAHA ALIZWA NA VIBAKA KISA CHIPS


Msanii wa muziki na mwigizaji, Baby Joseph Madaha, ‘Baby Madaha’ licha ya ukimya wa muda mrefu lakini bado anafanya vizuri na wimbo wake ‘Corazon’.

Baby Madaha, amejikuta akishikwa na butwaa baada ya kuporwa pochi yake na vibaka wawili waliokuwa katika pikipiki eneo la Makonde, Kunduchi, jijini Dar es Salaam. Mwigizaji huyo alipatwa na mkasa huo usiku wa juzi, wakati akielekea...
kununua chipsi karibu na kituo cha daladala cha Makonde. 

Ghafla pikipiki iliyokuwa na vibaka wawili walio pakizana ilipita kwa kasi karibu yake na kumpora simu mbili aina ya Samsung na mkoba uliokuwa na vipodozi, fedha na hati ya kusafiria.

Akipiga story na Mtanzania, Baby madaha alisema “Yaani hata sikuamini nilipo kutana na mkasa ule, nilikuwa nikitokea Uwanja wa Ndege nikielekea kwangu Makonde, lakini nikiwa kituo cha daladala Makonde nilihisi njaa, nika elekea kwenye banda linalouza Chipsi, ndipo nielekee nyumbani, lakini kabla sijafika katika banda wakaja watu wawili wakiwa wame pakizana katika pikipiki iliyokuja kwa kasi wakanipora mkoba wangu na kukimbia kwa kasi.

“Katika pochi yangu kulikuwa na simu mbili aina ya Samsung, dola 100 ambazo ni zaidi ya laki mbili, vipodozi na hati yangu ya kusafiria, lakini kwa bahati nzuri nilishika sura za wale vibaka na baada ya kutoa taarifa polisi ulifanyika msako mkali wakakamatwa wengi na nilipoitwa nilifanikiwa kuwatambua walionipora,” alieleza Baby Madaha.

Alisema baada ya utambuzi huo ulifanyika ukaguza katika nyumba wanazoishi vibaka na baadhi ya vitu, ikiwemo simu moja, vipodozi na dola 100 zikapatikana, upelelezi unaendelea kusaka vitu vilivyobaki, ikiwemo hati ya kusafiria, watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi.

Mbali na hilo Kwa sasa Baby Madaha na wasanii wenzake wawili, Isabella Mpanda na Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ wapo mbioni kuzindua wimbo wao mpya wa ‘Mario’ kupitia kundi lao la Scorpion Girl.

0 comments:

Post a Comment