Msanii wa filamu za kibongo, Kajala Masanja amevunja ukimya na kufunguka
kuhusu maneno yaliyokuwa yanazunguka mwa muda mrefu mitaani yakimtaja
kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda tangu akiwa DC wa kinondoni alipokuwa
akishirikiana kwa karibu na msanii huyo kwenye shindano la kusaka vipaji
vya wasanii wa Wilaya ya Kinondoni lililojulikana kama Kinondoni Star
Search.
Katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, Kajala alipoulizwa kuhusu
madai ya kuwa na uhusiano na Makonda, alijibu kwa haraka na kwa kifupi...:
“Hapana sijawahi kutoka naye kabisa. Hilo halipo.”
RC Makonda aliwahi kuzungumzia madai hayo akiwa bado Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, ambapo alisema ni propaganda zinazoelezwa na wabaya wake wa
kisiasa ambao wamekuwa wakisaka mbinu za kumchafua kila kukicha.
“Ni muda mrefu tu, walianza kipindi kile wakati wa Bunge la Katiba
nilipokwenda Bungeni na mwigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, wakasema
natembea naye, wakanyamaza. Sasa wamehamia kwa Kajala baada ya kufanya
naye kazi", alisema Makonda.
“Hakuna ukweli wowote wanatungatunga tu mambo, watakuwa na sababu zao
kwa sababu mtu kama Kajala, maneno yameibuka baada ya kufanya naye
project ya kutafuta vipaji vya wasanii.“
"Nimeshirikiana na wasanii wengi wa kiume katika project hiyo lakini kwa
kuwa wameona mwanamke ni Kajala peke yake, wanasema vitu ambavyo havina
kichwa wala miguu. Najua kuna wengine wanaoeneza haya mambo wanatumika
kisiasa lakini mimi sijali".
Monday, November 21, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment