Rapa
mkongwe kwenye muziki wa hip hop Tanzania King Crazy GK amefunguka na
kusema kuwa viongozi wengi wa Afrika kwa sasa hawana uzalendo wala utu
wametanguliza maslahi yao mbele kiasi cha kutojali wananchi na kupelekea
kuwaua watu wasio na hatia.
King Crazy GK alisema haya wihivi karibuni kupitia kipindi cha Planet bongo na kusema ndiyo maaana viongozi wengi wa Afrika wapo tayari kuona watu wanakufa ili wao...
waendelee kubaki madarakani na kuendelea kuongoza nchi ili hali labda hata wananchi hawawataki.
" Unajua viongozi wa sasa wengi ni wauaji, angalia viongozi wa nchi za Kiafrika wapo tayari kuona watu wanakufa ili wao waendelee kubaki madarakani, tofauti ni kipindi cha Mwalimu Nyerere au kipindi na viongozi wengine wa Afrika kama wakina Mandela ambao wao walikuwa wapo tayari kufa kwa ajili ya kuwalinda na kuwapigania wananchi wao, ndiyo maana unaona kiongozi kama Mandela alikuwa tayari kufungwa kwa ajili ya watu wake. Lakini viongozi wa saizi wanang'ang'ania madaraka wanatumia nguvu za dola kuwadhuru watu ili wao waendelee kubaki madarakani" alisema GK
0 comments:
Post a Comment