Msanii Mkoloni ambaye pia ni mkongwe kwenye game la bongo fleva,
amesema kitendo cha wasanii kutotoa album ni uoga wao na siyo ugumu wa
soko kama wanavyodai wengi wao.
Akizungumza amesema yeye anapingana na
kauli hiyo, kwani anaamini kila mmoja ana uwezo wa kutoa albam na...
kufanya vizuri.
"Kwa kusema kwamba albam haifanyi vizuri sana mimi hilo kidogo natofautiana, kila mtu anao uwezo wa kutoa albam basi tu kwa sababu watu wanaona kama vile utaratibu ambao ulikuwepo awali, kwa maana kwamba yule msambazaji ambaye alikuwa anapeleka albam na kudistribute, watu wanaona kama vile hafanyi hivyo tena, na hiyo ni kutokana na changamoto za kukua kwa teknolojia, pirates zimekuwa nyingi sana watu wanaona sheria hazifanyi kazi, mambo mengi yamelala", alisema Mkoloni.
Mkoloni amesema yeye binafsi hivi karibuni anatarajia kuja na albam yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Mipango Side B', baada ya kimya kirefu kwenye game ya bongo fleva.

0 comments:
Post a Comment