Pages

Subscribe:

Wednesday, November 16, 2016

MTANDAO WA TIDAL WAMWINGIZA JAY Z MATATANI


Record Label ya Prince PNG yamfungulia mashitaka rapper Jay Z kwa kuitumia album ya mwisho ya Prince katika mtandao wake wa kustream music wa Tidal.

Baada ya kupigwa chini na familia ya Prince kuhusu kumiliki nyimbo za Prince ambazo hazikuwahi kutoka, Jay z amekumbana na mkasa mwingine baada ya kutumia ngoma kibao za Prince katika...
mtandao wake wa Tidal bila makubaliano ambayo waliekeana na uongozi wa Prince.

Kupitia mtandao wa Tmz umeripoti kwamba Record Label ya Prince iliingia mkataba na Tidal pamoja na Roc Nation kustream album moja tu ya Prince ambayo ni ‘Hit N Run: Phase 1’, lakini cha kushangaza ni kwamba Tidal pamoja na Roc nation hawakufanya hivyo na kuamua kuziweka Album zote za Prince katika Tidal, ndipo uongozi wa Prince ukaamua kuchukua jukumu hilo la kumshitaki Jay z na label yake ya Roc Nation.

Bado label ya Prince, PNG haijaeleza inaitaji kiasi gani cha Fedha, ila mtandao wa Tmz umepata habari kwamba label ya Prince inaweza kudai fidia kubwa sana ambayo itazidi kuikandamiza Tidal.
Album ambazo zilitolewa na Tidal bila ya kibali kutoka label ya Prince ni hizi hapa ‘I Wanna Be Your Lover,’ ‘1999,’ ‘Little Red Corvette,’ ‘Cream,’ ‘Purple Rain,’ ‘Controversy,’ ‘Pop Life,’

0 comments:

Post a Comment