Lameck Ditto (kushoto) akiongea na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kulia). Mkali wa Bongo Fleva anayetikisa kwa sasa na wimbo wake ‘Moyo Sukuma
Damu’, Lameck Ditto, amesema yupo katika mchakato wa kurudisha
utaratibu wa albamu na katika albamu yake mpya upo wimbo alioshirikiana
na Mfalme wa Mashairi, Selleman Msindi ‘Afende Selle’.
Ujio wa albamu hiyo utamrudisha Afande Selle kwenye game na Ditto
anaamini msanii huyo ana uwezo mkubwa sana na mwenye...
heshima katika
sanaa. Kibao hicho kitamrudisha Afande Sele na ataweza kuwa bora kama
zamani.
Aidha Ditto ameendelea kutajwa kama mwandishi bora kutoka Jumba la
Vipaji Tanzania (THT) ambapo ameandika nyimbo nyingi kama vile ‘Malkia
Wa Nguvu’ wa Estelina Sanga ‘Linnah’ na nyingine nyingi.
0 comments:
Post a Comment