Video queen matata ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha redio moja
jijini hapa, Gift Stanford ‘Gigy Money’, ametema cheche akisema kuwa,
watu wote wanaomsema kwamba kutokana na kuvaa nusu utupu na kujiachia na
midume mbalimbali huenda ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi, waache
kwani kama ni kweli basi wengi wangekufa kwa sababu ameshatembea na
mastaa kibao Bongo.
Gigy Mone akizungumza juzi, Gigy alisema kwamba
amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali wakubwa Bongo
akiwemo Mbongo Fleva, Ali Kiba na...
kudai kuwa, kama kuambukizwa virusi
angeanza yeye na wengine wangefuata.
“Unajua watu wanashangaza sana. Kama mtu ana virusi vya Ukimwi hawezi
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu anayempenda, ningependa watu
waache unyanyapaa.
Ninachojua mimi sina Ukimwi kwa kuwa nilipima kwa
shinikizo la mpenzi wangu wa sasa (Moulad Alpha ‘Moj’) na watu
niliotembea nao wanaendelea vizuri tu, wengine wachumba zao
wananyonyesha,” alisema Gigy.
Video queen huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kuvaa nusu
utupu ni kitu anachopenda kufanya toka ndani ya moyo wake hivyo hakuna
mtu wa kumwambia kitu au kumkataza hata siku moja na wala siyo mgonjwa
wa akili bali anafanya kitu kujifurahisha nafsi yake si ya mtu mwingine.
“Mimi nasikilizaga moyo wangu unasema nini, si mtu anasema nini juu
yangu hivyo kama kuvaa nusu uchi wana hofu na mimi waondoe hilo kwa
maana kama ni Ukimwi wengi wangeondoka siku nyingi kwenye ramani ya
dunia hii maana hakuna niliyemuacha kwa mastaa unaowajua,” alisema Gigy
kwa kujiamini.
Gigy ameshatoka kwenye magazeti mbalimbali akidaiwa kutembea na
mastaa kama Hemed Suleiman ‘PHD’, Richard Martin Lusinde ‘Rich Mavoko’,
Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Seif
Shaban ‘Matonya’ na Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Mwingine aliyewahi kutajwa ni Mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’ na Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan.
Thursday, January 5, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment