Pages

Subscribe:

Sunday, January 1, 2017

RAIS MAGUFULI : HAKUNA KUPANDA UMEME... PIA AMTUMBUA MKURUGENZI WA TANESCO


 
Zikiwa zimepita siku mbili toka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeridhia ombi la Shirika la umeme nchini TANESCO la kupandishwa kwa bei ya umeme kwa asilimia 8.5 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
 
Mh. John Pombe Magufuli ameungana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kupinga hatua iliyochukuliwa na EWURA.
Rais Magufuli akiwa mjini Bukoba leo amesema suala la kupandishwa bei ya umeme lilikuwa ni suala la mtu mmoja kulingana na... nafasi yake na kwa kitendo hicho Rais anakiri kuwa bado kwenye Serikali kuna majipu meni na ataendelea kuyatumbua.
"Namshukuru sana Waziri wa Nishati na Madini ameshatengua maamuzi ya EWURA kwa hiyo umeme hakuna kupanda, haiwezekani unapanga mikakati ya kujenga viwanda na hasa katika mikakati hii mikubwa ya nchi ya kusambaza umeme mpka vijijini, na umeme huu unaenda mpka wa watu masikini walioubwa kwa mfano wa Mungu harafu mtu pekee kwa sababu ya cheo chako unakwenda unasimama na kwenda kupandisha bei ya umeme. 

Na ndiyo maana baba Askofu nalizungumza hili kwamba majipu bado yapo mengi na nitaendelea kuyatumbua " alisema Rais Magufuli 
Mbali na hilo Rais Magufuli amewaomba Watanzania waendelee kuwaombea kwani lengo la serikali anayoiongoza ni kwenda na wananchi wa chini 


Rais John Pombe Magufuli leo tarehe 1/1/ 2017 ametengua uteuzi  uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania 9TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba na kumteua Dk Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo. 

Akiwa mkoani Kagera leo Rais Magufuli alisikika akisema kuwa haiwezekani mtu mmoja kutokana na nafasi yake afanye maamuzi ya kupandisha umeme huku akitambua kuwa kufanya hivyo ni kuwaumiza watanzania na kuahidi kuendelea kuwatumbua wafanyakazi wa Serikali ambao ni majipu. 

Kwa mwaka 2017 Mkurugenzi wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba anakuwa mfanyakazi wa kwanza kutumbuliwa na Rais John Pombe Magufuli 

0 comments:

Post a Comment