Pages

Subscribe:

Saturday, January 21, 2017

HIZI NDIYO FAIDA ZA KULA NYANYA CHUNGU (NGOGWE)

mbuzi 2Nyanya chungu au ngogwe ni tunda ambalo wengi tumekuwa tukilitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika kunogesha mboga lakini wachache mno wanaojua faida zake kiafya.

Pamoja na kufanya mboga kuwa na ladha na harufu ya aina yake, nyanya chungu zina kazi kubwa katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na...
kujenga na kuimarisha afya ya mlaji.

Nyanya chungu ipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi vikiwemo vitamin A, B, na C ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi ya kuboresha afya ya mwili kwa ujumla.

Ndani ya nyanya chungu pia kuna Vitamin K inayosaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu.
Licha ya kuwa karibu asilimia 90 ya nyanya chugu ni maji, mboga hii ina madini ya chuma na potassium hivyo kusaidia uimara wa mifupa.

Nyanya chungu pia husaidia kuimarisha kinga ya mwilli na kumsaidia mlaji kuepukana na magonjwa ya mara kwa mara, Mboga hii pia ni kinga inayoweza kumuepusha mlaji kupata maradhi ya moyo au tumbo kujaa gesi au hutoa kinga kwa wanaume wasipate na ugonjwa wa ngiri.
 
Kwa wagonjwa wa kisukari, nyanya chungu ni dawa inayoweza kusaidia katika kupunguza kiwango cha sukari mwilini, hivyo basi katika chakula chako ni muhimu sana kula nyanya chungu japo kwa wiki mara mbili au tatu kutokana na faida zake kama tulivyoainisha hapa.

0 comments:

Post a Comment