Msanii
wa bongo fleva Madee amesema hajutii matusi yanayotukanwa kupitia
mitandao ya kijamii kuwa amepora simu kwa kuwa wanaomtukana hawaujui
ukweli na wakiujua watatulia.
Akionge kupitia eNewz Madee amesema hajapora simu bali alikuwa anadai pesa ambayo aliitoa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na badala yake haikufanyika jambo lililomfanya
aende kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kurudishiwa pesa yake, na
ndipo... hayo yakatokea.
"Baada ya kuona pesa yangu ipo tu imekaa
hafanyi kazi yoyote, nikafuatailia sheria, nikaenda polisi, nikasaidiwa
kupata haki yangu, nashukuru nimepata haki yangu, wala sijutii
kinachoendelea, sasa mi naweza kupora simu rafiki yangu, mi natumia simu
yangi iPhone 7 na hiyo simu nayoambiwa nimepora ni S4, halafu kama ni
kupora nisingeenda na polisi" amefafanua Madee
Pia Madee amesema pesa yake huwa haipotei hata kama ikiwa imechukuliwa na maiti.
Hata
hivyo Madee amesema uongo huwa hauishi muda mrefu hivyo hawalaumu wale
ambao wamemtukana kwa kuwa hawaujui ukweli na anaamini kuna siku watu
wote wataujua ukweli.
Friday, January 20, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment