Watu wengi hutumia tunda tu bila kujua kuwa si tunda pekee lenye manufaa kwa afya. Majani ya mpera ni mazuri kwa ajili ya ngozi, nywele na afya kwa ujumla, leo tuangazie faida ya majani hayo kwa... afya ya binadamu kwa kuyanywa kama chai.
Namna ya kuitengeza chai ya majani ya mpera ni rahisi. Kuna namna mbili, kwanza kwa kuchemsha maji kama glasi nne mpaka itokote sana, chukua majani kama 10 ya mpera, weka ndani ya yale maji moto alafu funika kwa dakika 10 – 15. Koroga chuja, weka kwenye kikombe, hapo chai itakuwa tayari kwa kuinywa.
Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani kama kumi yakiwa ndani, yachemke kwa dakika 10 -15, chuja tia asali badala ya sukari, chai tayari. Waweza kutumia majani ya mpera yaliyokaushwa pia.
Unaweza kutumia majani ya mapera kama chai na utapata faida 5 zifuatazo:
1.’Chai’ ya majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi, inasaidia madini ya carbohydrates yasigeuzwe kuwa sukari ndani ya mwili hivyo kupunguza hamu ya kula.
2.Chai ya majani ya mpera pia inashusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili kuondoa ‘insulin’. Kwa sababu hii, wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia mara kwa mara.
3.Chai ya majani ya mpera pia hupunguza lehemu mbaya (bad cholestrol) bila kudhuru lehemu nzuri.
4.Chai hii ina nguvu za kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa kuzuia magonjwa ya kuharisha na kipindupindu.
5.Chai hii inatibu mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na chakula chenye sumu.
0 comments:
Post a Comment