Kampuni hiyo yenye Makao Makuu yake
katika nchi anayoiongoza Rais Donald Trump, Marekani kwenye jiji la New
York na Ofisi Mjini Berlin, Cape Town na Buenos Aires, Napoleon atakuwa
na cheo cha pili kwa ukubwa baada ya...
Mkurugenzo Mtendaji (CEO), Dexter
Davis kwenye kampuni hiyo.
Moja ya majukumu ya Napoleon, atakuwa
akisimamia zaidi kazi za kampuni hiyo upande wa Afrika na Mashariki ya
Kati, japo hiyo haimaanishi kuwa hatohusika na masuala mengine ya
kampuni hiyo duniani kote.
Blues
“Hii ni fursa ya kipekee katika
hatua hii ya career yangu. D Street Media Group ni kampuni ya
kujitegemea inayokua kwa kasi ikiwa imeshika kila upande wa dunia. Ni
heshima kubwa kwangu kuendeleza biashara yetu katika masoko ya Afrika na
Mashariki ya Kati ambayo nayaelewa vyema,” amesema Napoleon.
Aliendelea, “Naamini kuna fursa
nyingi kwa kampuni ya Kimarekani kama D Street barani Afrika, na tukiwa
na washirika sahihi kutengeneza maudhui mazuri, tutafanikiwa Afrika na
hasa Marekani na nje ya nchi.”
Kwa upande wake, Davis alisema, “Ninafurahi
kuleta mshirika mchangamfu kama Ernest, sifa zake kama muigizaji na
mtayarishaji, kutamfanya awe rais mzuri. Kwa haraka amekuwa na jina
Tanzania, sehemu aliyozaliwa baba yake na ambako amekulia. Nimesikia
mambo ya kuvutia kuhusu Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, na
ninafurahi kuwa na Ernest ndani yetu kutuongoza katika mafanikio ndani
ya bara la Afrika,” alisema Davis.
“Kuhusu ukweli kuwa Ernest
anazungumza Kiswahili, Kirusi, Kiswidishi na Kiingereza, ni asset pia.
Ongeza hapo ukweli kuwa ni mtayarishaji anayetaka kuileta Afrika na
Waafrika kwenye jukwaa la dunia ni kitu ambacho kimenifurahisha na
kujivunia zaidi.”
D Street tayari ina uwepo wake barani
Afrika ikiwa na ofisi Cape Town, Afrika Kusini. D Street Pictures, tawi
la utayarishaji, lilitayarisha filamu ya Afrika Kusini, iitwayo ‘Musiek
vir die Agtergrond,’ filamu ya Kiafrikaan iliyowekeza mwaka 2013.
Kampuni sasa ipo kwenye utayarishaji wa
mwanzo wa filamu iitwayo ‘The Blue Mauritius.’ Muingozaji wa Uingereza,
Charles Henri Belleville, (Jet Trash, The Inheritance) ataiongoza.
Belleville amemaliza kuongoza filamu yake ya pili na mtajwa wa tuzo za
Oscar, Tom Hardy (Mad Max, Legend).
Kisa cha filamu ya ‘The Blue Mauritius’
kinawahusu wezi watano wa kimataifa wanaoenda Cape Town kuiba muhuri
wenye thamani zaidi duniani. Filamu hiyo imekusanya mastaa duniani
akiwemo muigizaji wa Marekani, Eric Dane (Grey’s Anatomy, Last Ship),
Brian Cox (The Rise of the Planet of the Apes, The Bourne Supremacy),
John Ryes-Davies (The Lord of the Rings, Raiders of the Lost Ark) nguli
wa Ufaransa, Gerard Depardieu (Life of Pi, The Man in the Iron Mask),
kutaja wachache tu.
‘The Blue Mauritius’ itatengenezwa Cape
Town na katika mji mdogo wa pwani, Port Shepstone, Afrika Kusini. Ni
filamu iliyolenga soko la kimataifa lakini yenye kisa cha Kiafrika.
Mastaa wa Afrika Kusini akiwemo Pearl Thusi na Lwandle Ngwenya, nao
watashiriki.
Hiyo ni sehemu ya harakati za D Street
kuendeleza na kutayarisha filamu za biashara za Kiafrika zitakazosafiri
dunia nzima na kutengeneza mastaa wa Kiafrika. Ikiwa na kampuni ya
utayarishaji na usambazaji yenye makazi yake Marekani, inafanya hili
liwezekane zaidi. Filamu hiyo inatayarishwa na Davis pamoja na rapper,
muigizaji na mtangazaji wa Marekani, Nick Cannon (Chi-Raq, America’s Got
Talent).
0 comments:
Post a Comment