Upepo mwanana bado unaendelea kumpuliza, staa namba moja wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ baada ya mgombea anayewakilisha Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Omolo Odinga, kudaiwa kumuita nchini humo.
Kwa mujibu wa chanzo kisicho na chembe ya shaka, Kiba anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Seduce Me, alipata mwaliko huo mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni saa chache mara baada ya...
Odinga kushinda kesi ya uchaguzi Katika Mahakama ya Juu aliyokuwa amemfungulia Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye mambo yalimuwia mazito.
Kenyatta alitangazwa mshindi wa nafasi ya urais na Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IBEC) katika uchaguzi uliofanyika nchini humo Agosti 8, mwaka huu ambapo Odinga alifungua kesi hiyo mahakamani. Baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote, iliufuta uchaguzi huo kwa kueleza kuwa tume ya uchaguzi haikuzingatia uadilifu.
ODINGA KICHEKO
Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa mahakamani, Odinga alizungumza na wanahabari na kueleza hisia zake akisema alifurahishwa kwa kitendo cha mahakama hiyo kutenda haki hivyo kuwataka wapiga kura wake kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika baada ya siku 60 tangu hukumu hiyo itoke.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo hicho makini kilicho karibu na Kiba, uongozi wa NASA ambao ulimtumia Kiba katika kampeni za uchaguzi wa awali, haraka ulimtumia mwaliko kwa ajili ya pati maalum ya kusherehekea hatua ya ushindi huo nchini Kenya.“Yaani Kiba nyota inazidi kumuwakia. Baada tu ya Odinga ‘kumgaragaza’ Kenyatta kortini, wamemuita Kiba haraka sana ili aende kusherehekea nao ushindi huo. Si unajua tena alikuwa sehemu ya watu waliompigia kampeni Odinga katika uchaguzi uliopita?” Kilinyetisha chanzo hicho.
Katika mazungumzo yake na Ijumaa Wikienda, chanzo hicho kilizidi kushusha ubuyu kuwa kutokana na umuhimu wa Kiba na kazi kubwa aliyoifanya wakati wa kampeni, NASA waliamua kumtumia Kiba ndege binafsi (private jet) ili awahi sherehe hiyo ya kukata na shoka na ikiwezekana wafanye mazungumzo ya ‘kuliamsha dude’ la shoo kampeni.
0 comments:
Post a Comment