Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Seduce
me' ameamisha mashambulizi yake upande wa bongo movie na kuwaambia hali
mbaya waliyokuwa nayo katika kipindi hiki ni kutokana na kutokuwa na
umoja baina yao.
Alikiba
ameeleza hayo baada ya kuwepo tetesi ya baadhi ya wasanii wa bongo
movie kuwa wanashindwa kusaidiana katika kazi zao na...
kuogopana jambo
ambalo linaleta makundi kati yao na kuwafanya kushindwa kuwa kitu
kimoja.
"Mimi siku zote
nitawapigania bongo movie kwa sababu wakishafanya kazi zao na kuzipeleka
sokoni kwa ajili ya kufanya mauzo ndiyo basi tena lakini sisi
wanamuziki tunauwezo wa kufanya 'show' ambazo zitatulinda sisi hata kama
wananchi wamesikiliza ngoma zetu na kuzi-download bila malipo hatuwezi
kupata hasara kwa kuwa tunategemea show ambazo ndiyo zinalipa, kwa hiyo
umoja ni kitu cha msingi sana na ndiyo maana wenzetu wa Nigeria
wanasaidiana katika mambo yao na siyo kwamba wanaogopana", amesema Alikiba.
Pamoja na hayo, Alikiba aliendelea kwa kusema "Mimi
binafsi ningefurahi sana kama wasanii tungekuwa na umoja, sisi ni
wamoja siyo lazima mpaka tukutanishwe kwenye janga fulani!", amesisitiza Alikiba.
Kwa upande mwingine, Alikiba aliendelea
kuwashauri wasanii wenzake kuendelea kusaidiana kwa kuwa ni jambo zuri
ambalo anaamini litaweza kuwatoa sehemu moja na kwenda sehemu nyingine
kwa wasanii wote kwa ujumla bila ya kujali aina ya kazi anazozifanya.
0 comments:
Post a Comment