Aliyekuwa msanii kutoka kundi la 'The Industry' kabla ya kuondoka na
kuanza kuimba nyimbo za injili, Seline amesema kuwa kamwe mavazi yake
hayawezi kutafsiri kwamba wokovu wake haujakamilika kwa kuwa anaamini
hakufanya kuwaonyesha wanadamu bali Mungu
Seline
amelazimika kuzungumza hayo baada ya watu kuhoji sana kuonekana akiwa
tofauti kimuonekano na waimbaji wengine wa nyimbo za injili, ambapo
anaonekana...
kujiachia sana kimavazi.
"Kusema nimeokoka haina
maana kuwa natakiwa kumuonyesha kila mtu kwamba mimi ni mlokole.
Ninachoamini kwamba kuokoka ni kuokolewa nafsi na pia namtumikia Mungu,
naisaidia jamii yangu. Naishi jinsi ambavyo ametuagiza. Naamini kwamba
sipo asilimia 100 sahihi lakini najitahidi" Seline.
Wapo wapendwa ambao najua wanajaji
mionekano lakini kwangu mimi hapa wala sijali kwa sababu kama naishi
vile ambavyo naona nisahihi basi sitojali watu wakiongea.
"Seline ameongeza kwa kuwa
yeye ni kijana na ameamua kumtumikia Mungu basi inamlazimu kuishi kama
kijana hata akifika kuwaelimisha wamuelewe na siyo awaendee kwa nia ya
kuwaogopesha". ameongeza
Kwasasa wimbo wa Seline unaojulikana
baada ya kuondoka lebo ya inayosimamiwa na Nahreel pamoja na Aika 'The
Industry' ni 'Jitume' ambapo mwenyewe anauita 'Inspiration Song'
0 comments:
Post a Comment