Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunguka na kuomba muongozo wa
Spika kuhusu hali ya usalama wa nchi, kwa kuwa matukio ambayo
yanaendelea kutokea ya kihalifu hayana hitimisho yake.
Bashe
amesema hayo wakati akiomba muongozo ndani ya bunge kwa kumtaka Spika
wa bunge Job Ndugai kukubali ombi la kamati ya usalama ya bunge likutane
na...
vyombo vya usalama ili yaweze kupatikana majibu ya matukio
yanayoendelea kutokea.
"Mhe. Spika katika taifa
letu katika kipindi cha muda mrefu kumekuwa yakitokea matukio mbalimbali
ambayo sisi kama wawakilishi wa wananchi tuna wajibu wa kupata taarifa
sahihi juu ya muendelezo wa matukio hayo ambayo hayana hitimisho", amesema Bashe.
Pamoja na hayo, Bashe ameendelea kwa kusema "sisi
tunawaakilisha Watanzania milioni 50 lakini matukio haya yanayotokea
yanaharibu heshima ya taifa letu ningekuomba kama utaridhia na wabunge
wataniunga mkono, uitake kamati yako ya ulinzi na usalama ya bunge
tukufu ikutane na vyombo vya ulinzi na usalama ili tuweze kupata taarifa
kamili juu ya mambo haya yanayoendelea katika taifa letu, ili
Watanzania na sisi wabunge tuwe na uhakika kwa sababu hali inavyoendelea
hakuna mtu mwenye uhakika na maisha yake ya kesho. Dhamana tuliyopewa
sisi dhamana ya kusimamia mali, usalama pamoja na raia wa nchi hii", amesisitiza Bashe.
kwa upande wake Spika wa Bunge Mhe. Job
Ndugai amekubali hoja iliyotolewa na mbunge Bashe na kutoa amri ya kwa
kamati ya ulinzi na usalama ya bunge iende kukutana ili wapange ni jinsi
gani ya kulishughulikia jambo hilo na watakapokuwa tayari kabla bunge
kuhairishwa siku ya Ijumaa wiki ijayo warudishe majibu kwa bunge juu ya
walichoamua.
0 comments:
Post a Comment