Muigizaji wa filamu bongo, Haji Mboto ambaye ni shabiki wa Yanga
amewapiga vijembe watani wao wa jadi klabu ya Simba kuwa licha ya kuanza
kwa kishindo Ligi Kuu Bara kwa kuwanyuka Ruvu Shooting bao 7-0 bado
uhakika ubingwa utaelekea jangwani.
Mboto
ambaye mara kwa mara amekua akionekana kuikejeli Simba katika mitandao
ya kijamii amesema wao ndiyo mabingwa wa kihistoria wa ligi na hata...
wakianza kwa kutoa sare huwa wanamaliza ligi kwa ubingwa kama
walivyofanya msimu uliopita.
Amesema kwamba msimu uliopita Azam Fc
walitwaa Ngao ya Jamii lakini mwishoni mwa msimu Yanga ikatwaa
ubingwa,lakini msimu huu Simba wametwaa Ngao ya Jamii vivyo hivyo lazima
ubingwa utatua kwao ukiwa ni wa msimu wa nne mfululizo.
Aidha ameenda mbali zaidi kwa kusema
kwamba wao kama Yanga hawataki kuwa kama Rais wa Burundi Piere
Nkurunziza hivyo pindi watakapotwaa ubingwa msimu huu watakaa chini na
wanachama wenzao ili kuamua kuwaachia wapinzani wao ili wapate nafuu ya
kuchekwa mitaani.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa VPL
walianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Lipuli FC ya mkoani Iringa
huku Simba ikiiunguruma kwa ushindi wa jumla ya bao 7-0 dhidi ya Ruvu
Shooting na sasa inaongoza katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania
Bara.
0 comments:
Post a Comment