
Ben Pol amesema yeye kwa sasa anataka watu wamuone kama Mfalme wa R’n’B ndiyo maana ameamua kuchukua kifimbo hicho na...
kutembea nacho.
“Hii fimbo kwanza.. unajua saa nyingine unawambia watu kuwa mimi ni King wa R’n’B, lakini hii fimbo nililinua kwa ajili ya photoshoot halafu nikaipenda nikaamua niitumie kama props kwenye mitoko yangu na show zangu.“amesema Ben Pol kwenye mahojiano yake na Times FM, alipoulizwa sababu ya kutembea na kifimbo hicho.
Ben Pol ni moja kati ya wasanii wakali kwenye miondoko ya muziki wa R’n’B nchini Tanzania, na kwa sasa anatawala anga la Muziki na wimbo wake mpya wa ‘Kidume’.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment