Pages

Subscribe:

Saturday, September 9, 2017

DOGO JANJA: NASHUKURU MUNGU NIMETIMIZA NDOTO YA KUPIGA PICHA NA ALIKIBA



Msanii wa Bongo Flava kutoka kundi la Tip Top Connection, Dogo Janja hatimaye amefanikiwa kutimiza moja ya ndoto yake.

Dogo Janja anayehit na ngoma ya ‘Ngarenaro’ amefunguka hayo baada ya kukutana na mkali wa ngoma ya ‘Seduce Me’, Alikiba na kupiga naye picha. Kupitia mtandao wa kijamii wa insta dogo Janja amepost picha akiwa na alikiba na kuandika...


“Alhamdulilah leo nimetimiza ndoto yangu ingine yakupiga picha na alikiba @officialalikiba #Ngarenaro Link In My Bio,” ameandika Jajaro baada ya kukutana na Alikiba jijini Arusha.
Alikiba na Dogo Janja ni moja ya wasanii watakoshambulia jukwaa la muziki la Fiesta linalotarajiwa kuanza rasmi katika Mkoa wa Arusha hapo kesho Jumamosi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

0 comments:

Post a Comment