Pages

Subscribe:

Saturday, September 2, 2017

Story: NILILALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI - 12

SITASAHAU NILIPOLALA NA MWANAMKE JUU YA KABURI (12)
ILIPOISHIA JANA…
“Boboooooh!” ilipigwa honi. Tukaingia ndani ya gari. Nilimkuta yule dada jirani yangu amekaa kajiinamia. Nilitambua kilichomtesa. Muda wote wa safari alikuwa akichezea simu. Sasa simu ilichukuliwa na wajinga wale. Ili Kuepusha kuwa sehemu ya matatizo yake, sikumsemesha.

ENDELEA KUSOMA...

Safari iliendelea salama salmini na hatukukutana na tatizo jingine. Saa kumi na moja jioni tulifika mkoani Kigoma. Haikuwa mara... yangu ya kwanza kuwa katika mkoa huu, niliufahamu vyema.


Nililala katika nyumba ya kulala wageni maeneo ya Mwanga. Kwa kuwa nilichoka sana, niliamka saa saba mchana.

Sikufahamu ni wapi ningempata mzee Samike. Aliyenielekeza hakunipa maelezo kamili. Mambo yakawa magumu.

Hata hivyo sikukata tamaa. Saa nane mchana nilitoka kwenda kumtafuta mzee nisiyemfahamu japo kwa sura tu. Nilianza msako wa barabara kwa barabara. Kila mpita njia niliyekutana naye nilimwuliza: “Unamfahamu mzee Samike? Ana nywele nyeupe, ndevu nyeupe, sharubu nyeupe, nyusi nyeupe… pia amejaa misuli.” Wote walijibu: hapana. Nikarudi katika chumba changu niliyejaa uchovu na unyonge
Safari iliendelea salama salmini na hatukukutana na tatizo jingine. Saa kumi na moja jioni tulifika mkoani Kigoma. Haikuwa mara yangu ya kwanza kuwa katika mkoa huu, niliufahamu vyema.
Nililala katika nyumba ya kulala wageni maeneo ya Mwanga. Kwa kuwa nilichoka sana, niliamka saa saba mchana.
Sikufahamu ni wapi ningempata mzee Samike. Aliyenielekeza hakunipa maelezo kamili. Mambo yakawa magumu.
Hata hivyo sikukata tamaa. Saa nane mchana nilitoka kwenda kumtafuta mzee nisiyemfahamu japo kwa sura tu. Nilianza msako wa barabara kwa barabara. Kila mpita njia niliyekutana naye nilimwuliza: “Unamfahamu mzee Samike? Ana nywele nyeupe, ndevu nyeupe, sharubu nyeupe, nyusi nyeupe… pia amejaa misuli.” Wote walijibu: hapana. Nikarudi katika chumba changu niliyejaa uchovu na unyonge.
Siku iliyofuata nikaamua kuendesha msako wa nyumba kwa nyumba. Nilianzia Mwanga, nikapita kila kona. Sikumwona. Nikaongeza mitaa miwili zaidi, Gungu na Kikungu, lakini kote huko sikufanikiwa kumuona niliyemhitaji.
Uchovu ulinikamata nikaamua kurudi chumbani kwangu kupumzika. Nilipolala niliota ndoto zilizosimama katikati ya kukata tamaa na kuendelea na zoezi la kumtafuta Samike. Pia, mara tatu niliota nikikimbizwa na yule mtu wa ajabu. Nikapiga makelele yaliyowashtua wazinzi waliokuwa jirani ya chumba changu. Walipogundua ni makele ya mtu aliyeota, wakanipuuza wakiendelea kuyafaidi maumbile.
Kulikucha. Nikaamka na kuuanza msako. Kazi yangu ilikuwa moja tu, kumtafuta Samike, nimwombe radhi ili aniondolee balaa la kufukuzwa na jitu lile la kutisha.
Leo niliamua kwenda kumtafuta Katubuka. Huko ni mahala ambako palikuwa na wavuvi wengi. Niliwaza bila shaka mzee aliamua kuwa mvuvi. Nilijipa matumaini kuwa huenda nikampata huko. Nilipanda gari la kwanza nikashuka nilipopataka. Nikachukua la pili ambalo lilinipeleka moja kwa moja mpaka Katubuka.
Nilijitahidi kuangaza taratibu kuona kama ningemwona mzee. Sikumwona, wavuvi wengi walikuwa vijana na wazee wachache ambao hawakuwa na sifa za mzee Samike.
Hata hivyo, kama ilivyokawaida yangu huwa siachi kuwauliza watu kuhusu mzee Samike. Nikamfuata kijana ambaye alikuwa akinitazama muda wote tangu nifike eneo lile.
“Kaka habari yako!” nilimsabahi. “Salama.” “Unamfahamu mzee mmoja anaitwa Samike? Ana nywele nyeupe, nyus…” kabla sijamaliza kuzungumza, kijana alibadilika na kuwa yule mtu wa ajabu aliyekuwa akinifukuza. Nikaanza kukimbia.
Nini hatma ya mbio hizi? Tukutane kesho…

0 comments:

Post a Comment