Malkia wa filamu bongo, Wema Sepetu amekanusha kuwa na mahusiano na
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe ambaye miezi michache iliyopita
alihusishwa kutoka naye baada ya sauti zinazodhaniwa kuwa za
kwao kusambaa mitandaoni.
Wema
amesema kuwa katu hajawahi kuwa na mahusiano na kiongozi huyo wa
upinzani kwani ni mtu ambaye anamuheshimu sana na kuongeza kwamba sauti
hizo...
zenye mazungumzo ya faragha zilitengenezwa na watu asiowafahamu
wenye nia ya kumchafua.
Akifanya mahojiano na Mtangazaji wa
Nirvana, Deogratius Kithama, Wema Sepetu amesema anashindwa kuelewa
sauti hizo zilipotokea kwani anamuheshimu sana Mh. Mbowe na heshima
yake hiyo wakati mwingine inampa hali ya kumuogopa hivyo anaamini
kitendo hicho kilitengenezwa na watu wenye nia ya kuwachafua kisiasa.
"I was shocked, sijui
chochote kuhusu hicho kitu. Mimi mwenyewe sijui kilipoanzia na kwanza
ninavyomuheshimu yule baba mpaka namuogopa sasa hili lilipotokea i was
like hizi ni figisu. Ingawa sijakutana na Mbowe toka jambo hili kutokea
kwa sababu yupo busy lakini viongozi wengine wa CHADEMA walinielewesha
ni kwa nini watu wanafanya hivyo. Wema Sepetu
Wema ameongeza " Unajua hizi ni siasa.
Huku ni upinzani na wengine ndiyo wapo madarakani so mambo kama haya ya
kisiasa yanatokea ingawa huyo aliyetengeneza sauti kufanana na ya
kwaangu yupo vizuri sana.
Sauti ya Wema pamoja na Mbowe
ilivujishwa miezi michache baada ya muigizaji huyo pamoja na mama yake
kuhamia upinzani wakitokea CCM kwa madai ya kutaka kutumikia chama
chenye demokrasia ya kweli
0 comments:
Post a Comment