JUNI 2015 wakati Manchester United ikiivaa Southampton
katika mechi ngumu ya Premier League alikatisha panya uwanjani. Hii
ilisababisha malalamiko makubwa kwa mashabiki kwa kuwa lilionekana ni
kama jambo la aibu kwa klabu.
Januari 2016, Kocha Louis van Gaal alilalamika kwamba
utengenezaji wa uwanja sehemu ya kuchezea yaani pitch ulikuwa unachelewa
licha ya klabu kutoa... pauni 800,000 (Zaidi ya Sh bilioni 2.3). Wakati
mwingine wanalazimika kuchelewa kufanya mazoezi kwa kuwa kunakuwa na
mambo ya matengenezo.
Suala la uwanja huo wa kuchezea kuonekana una matatizo
lilionekana kuukerea uongozi na Bodi ya Manchester United ambayo kikubwa
inachotaka ni kulinda heshima ya klabu hiyo maarufu kuliko zote England
na moja ya klabu tatu kubwa zaidi duniani, nyingine mbili zikiwa ni
Real Madrid na Barcelona zote za Hispania.
Baada ya hapo, aliyepewa fedha kwa ajili ya kazi hiyo
akahimizwa na yeye akafanya kweli na awali, ilionekana ulitakiwa kuwa
kama ule wa Wembley ambao ni mali ya Serikali ya Uingereza lakini safari
hii, pitch ya Old Trafford inaonekana ndiyo bora zaidi England na
ikiwezekana Ulaya zima pia inawezekana kufananishwa na ile iliyo katika
Uwanja wa Emirates pekee,Uwanja wa Emirates unamilikiwa na wapinzani
wakubwa wa Man United hawa ni Arsenal walio katika Jiji la London.
Msimamizi wa uwanja huo bwana Allah Smith ambaye anasema
pitch yao ndiyo bora zaidi duniani kwa kipindi hiki kutokana na
teknolojia mpya,Akasema hata kwa huduma inakuwa tofauti kwa kuwa
Manchester United na Arsenal ndiyo timu zilizoanza kutumia teknolojia
mpya ya majani ya kawaida au asili wenyewe wanasema natural kuchanganywa
na yale ya bandia.
Unajua kuna viwanja vya asili kama Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam na ule wa bandia kama ulivyo wa Uhuru lakini nyasi
za Old Trafford ni asili asilimia 97 na asilimia 3 ni bandia na hii ni
kuyafanya majani kuwa imara zaidi na mfumo mpya unaowafanya wachezaji
kuwa salama zaidi.
Lakini kama hiyo haitoshi, uwanja huo kwa chini una
mabomba maalum yenye uwezo wa kutengeneza joto kunapokuwa kipindi cha
baridi au kuwa ya baridi sana kunapokuwa kipindi cha joto kali ili
kuufanya uwanja kuwa na hali ya hewa isiyowapa tabu wachezaji,Katikati
uwanja huo umeinuliwa kwa inchi nane ili maji ya mvua yamwagike pembeni
kutowasumbua wachezaji wakati wa mechi au kipindi cha mvua kubwa,Mabomba
ya plastiki yaliyozungushwa chini ya uwanja huo yana urefu wa Kilomita
37 kama yatanyooshwa moja kwa moja. Ukubwa wa pitch ya Old Trafford goli
hadi goli ni mita 105 na upana ni mita 68.
Mara ya kwanza uwanja huo Old Trafford kufanyiwa
marekebisho ilikuwa ni mwaka 1999 baada ya Man Unted kushinda makombe
matatu likiwemo la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha Sir Alex Ferguson
akataka ufanyiwe marekebisho makubwa ili kuwapa nafasi ya wachezaji
kupambana vema wakiwa nyumbani,Klabu ikamwaga pauni 250,000 (zaidi ya
Sh milioni 716) na ukarabati mkubwa ukafanyika na kuanzia hapo
haukufanyika tena hadi msimu huo wa 2012-13.
0 comments:
Post a Comment