Pages

Subscribe:

Saturday, August 1, 2015

SARMY CLEVER: SINA BEEF NA BARAKA DA PRINCE, NA SINA MAHUSIANO NA...

Ukizungumzia wasanii wanao fanya vizuri ktk tasnia ya muziki wa bongo huwezi kumsahau mkali wa kibao cha Tausi si mwingine namzungumzia Sarmy Clever, Baada ya kimya cha muda mrefu leo ktk kipindi cha Hot In Hot cha SmashKilimanjaro kinacho kujia kila siku ya jumamosi leo tumekutana na Sarmy na Kufanya naye Interview nakuzungumzia mengi ikiwemo kuhusu kufanya Video yake mpya na Hanscan, beef kati yake na Baraka Da Prince, pia...
kuhusu scandal yake ya kutoka na video Queen.

Kutokana na mfurulizo wa kupost picha za mwanadada ambaye hakuweza kutambulika jina tuliamua kumtafuta sarmy clever na kuzungumza naye machache, Baada ya kupost picha hiyo hapo juu na kuandika maneno yaliyo someka kama SITAKI MZOZO... ANIMALIZAEEEE.. na mwisho kuweka alama ya pete (kama unavyoona pichani), Alipo ulizwa ni nani Sarmy alidai kuwa huyu ni Video Queen
Alipo uliza jina la video queen huyo Sarmy hakutaka kutaja jina lake..

Beef Na Baraka Da Prince
Siku za nyuma baada ya tuzo za kili Sarmy alipo ulizwa anazungumza nini kuhusu Baraka.. Sarmy alisema hamkubali huyu jamaa hata kidogo lakini alipo ulizwa kama kuna tofauti kati yake na Baraka alijibu kuwa Sina Beef na Msanii yeyote na kumkubali mtu ni Hiari yako.
vipi sasa kama humkubali mtu huyu mbona umetumia moja ya neno ambalo lipo kwenye ngoma yake mpya?? (Sitaki Mizozo)
Sarmy: Staki mzozo ni neni la Kiswahili mm mtoto wa uswazi!!!!!

KUSHOOT VIDEO KWA HANSCAN
Kuna Directors wengilakini wewe umeonekana kumtafuta Hanscan nini kilicho kuvutia kwake au kwa kuwa amefanya video na msanii mkubwa hapa Tz?? (Diamond)
Sarmy: Hapana natarajia kufanya kazi na directors wengi ila kwa sasa nimeona nianze tu na huyu Hanscan.

MAADILI YA DINI 
Sarmy ameonekana ktk picha zake akiwa amejitupia cheni mbali mbali zenye vionjo vya dhahabu ambazo kwa maadadili ya dini yake hairuhusu kuvaa vitu hivyo kwani husemekana kama ni haramu na alipo ulizwa sarmy alisema: Cheni ninazoo vaa ni zakawaida na amini ni zakiume.

KUHHUSU WIMBO MPYA
Sarmy alimaliza kwa kusema kuwa anatarajia kuachia ngoma mpya hivi karibuni ambayo ameshirikiana na msanii mkubwa wa hapa bongo hivyo aliomba mashabiki zake mkae tayari kwa kupata kitu kipya japo hajaweka wazi ni nani anaye fanya naye ngoma hiyo mpya.

0 comments:

Post a Comment