Producer
mkongwe wa muziki wa Bongo Flava Master Jay, amesema tuzo
wanazoshiriki wasanii wetu nje ya nchi haziwasaidii katika kutanua wigo
wa kibiashara wa msanii wa Tanzania huku wakitumia ghara kubwa
kutengeneza video zenye ubora ili...
kujitangaza kimataifa.
Master Jay ametoa kauli hiyo alipokuwa akiongea kwa njia ya simu kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kuleza kwa undani suala hilo.
"Kusema kweli sijaona inatusaidia nini, ukiniuliza mimi mtu wa lebo, unafanya video kali ili ipigwe kwenye station za nje za televishheni ili upanue soko, hiyo ndo lengo kuu kwamba tayari sawa nimeshaweka such record hapa Tanzania Mungu Kanibariki, je, nitaingiaje Mozambiki, Zambia, Zimbabwe na kadhalika, naona video zinafanyika wanaalikwa kwenye tuzo, lakini sioni mtu akiwa anafanya za show tofauti na zile alizokuwa akizifanya kabla", alisema Master Jay.
Master Jay aliendelea kwa kusema kwamba ingawa anaona promo zinafanyika, lakini hawaalikwi kwenye show za kimataifa kama wasanii wa Nigeria, havyo hajaona inatusaidia nini kwa sisi Watanzania.

0 comments:
Post a Comment