Sunday, September 6, 2015
STORY: PETE YA JINI SABRAH - EPISODE 8
PETE YA JINI SABRAH - 8
Mtunzi : Mwinyi Mvua
0789 569355
Ghafla nilimuona mama sophia akibebwa na kundi la majirani wakimpeleka ndani hakika mama sophia alionekana mtu aliekuwa akipo teza fahamu mara kwa mara hatimaye safari ya kumpeleka baba sophia ikaanza kuelekea mzenga nilijaribu kuangaza pande zote yule mwana mke mwenye IJABU sikuweza kumuona tena pale msibani ingawa...
hofu kubwa ikiwa ime tawala moyoni.
Safari yetu kuelekea mzenga ilichukua Li saa 1 na 30 hatimaye tulifanikiwa kumpumzisha baba sophia kwenye nyumba yake ya milele " kwani nini kilicho muua marehemu?? " mtu mmoja alisikika pale makaburini huku akionekana mwenye shahuku ya kutaka kujua ukweli" Mimi mwenyewe sifahamu ila?? " Mtu mwingine alisikika akisema watu wale hakika nilivyowa angalia vizuri taswira ikanijia kuwa watakuwa ni ndugu wa marehemu baba sophia.
Hatimaye miezi ilikatika tangu tumzike marehemu baba sophia siku moja wakati nipo chumbani kwangu nakumbuka ilikuwa kama saa 7 mchana gafla nikahisi usingizi sikujua usingizi ule hata ulipotokea ulikuwa wa ma ajabu kwa namna moja wakati nipo kwenye usingizi gafla nika muona binti mzuri wa kiarabu aki ingia chumbani kwangu binti yule alielekea moja kwa moja hadi kabatini mkononi mwake alionekana ameshika pete iliyo onekana ika ng'ara muda wote.
Binti yule akaiweka pale kabatini kisha akaja kitandani kwangu nilipo lala binti yule taratibu aka anza kuni papasa kifua changu gafla!! Nika kurupuka kutoka usingizini cha kushangaza niliona upepo mkali uki peperusha pazia huku mlango wangu ukionekana ukiwa wazi wakati hapo awali niliusindika nilínuka haraka kuelekea nje kuangalia vizuri labda kuna mtu aliingia kutoka pale ukumbini nilimkuta mama sophia akiandaa chukula cha mchana.
" Eti jirani ujaona kitu muda huu hapa?? " nilimu uliza mama sophia huku nikiwa tumbo wazi " kitu gani tena saidi?? " Sauti ya mama sophia ilisikika huku akiendelea kukata vitunguu " kitu chochote jirani?? " nilimu uliza tena mama sophia " Hapana sija ona chochote " mama sophia alinijibu huku akiendelea na shughuli zake pale jikoni " Sawa usijali " nilimwambia mama sophia huku niki ingia chumbani kwangu.
Mama sophia alionekana kukichunguza kifua changu muda wote nilirejea hadi pale kitandani maswali mengi yalinijia kichwani mwangu pasipo kupata majibu gafla...
ITAENDELEA
Labels:
LOVE & STORY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment